Rwanda yaingiza mabasi yanayotumia umeme ili kuhimiza maendeleo ya usafiri usiochafua mazingira

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 26, 2023

Tarehe 29, Machi, 2022, wanafunzi wa Kigali, Rwanda wakisubiri kupanda basi la kurudi nyumbani kwa ajili ya likizo . (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)

Tarehe 29, Machi, 2022, wanafunzi wa Kigali, Rwanda wakisubiri kupanda basi la kurudi nyumbani kwa ajili ya likizo. (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)

Hali mpya imetokea barabarani huko Kigali: Magari mapya yanayotumia umeme yanapita kati ya magari ya jadi yanayotumia mafuta.

Mamlaka ya Mji wa Kigali ikifanya ushirikiano na kampuni ya Kenya BasiGo, imefanya majaribio kwa mabasi madogo madogo na kuanzisha majaribio ya mabasi yanayotumia umeme katika huduma ya usafiri wa kiumma ya mji huo mapema ya mwezi huu.

Baada ya kuchajiwa kwa kutosha, basi la aina hiyo litaweza kuendeshwa kwa kilomita 300. Kituo cha kuchaji kipo kwenye mtaa wa Kicukiro wa Kigali.

Ofisa mhusika alisema kuwa, lengo lao ni kuingiza mabasi 200 kwenye usafirishaji wa barabarani mjini Kigali ndani ya miezi 18, ambayo kila basi litaweza kubeba abiria 70.

Wakazi na wataalamu wa Rwanda walisema, huduma hiyo ya mabasi yanayotumia umeme itahimiza juhudi za nchi hiyo za kuendeleza mfumo wa usafiri wenye akili bandia, na kuhimiza maendeleo endelevu ya uchumi.

Mwezi wa Julai, serikali ya Rwanda ilisaini makubaliano na kampuni ya Vivo Energy, na kuingiza mabasi zaidi ya 200 katika nchi hiyo.

Tarehe 29, Machi, 2022, wanafunzi wa Kigali, Rwanda wakisubiri kupanda basi la kurudi nyumbani kwa ajili ya likizo . (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)

Watu wakipanda baiskeli ya kiumma katika eneo la kiini la kibiashara mjini Kigali, Rwanda tarehe 9, Septemba, 2021. (Picha na Cyril Ndegeya/Xinhua)

Picha iliyopigwa tarehe 10, Mei, 2019 ikionesha mandhari ya Kigali, Mji Mkuu wa Rwanda. (Picha na Lv Tianran/Xinhua)

Picha iliyopigwa tarehe 10, Mei, 2019 ikionesha mandhari ya Kigali, Mji Mkuu wa Rwanda. (Picha na Lv Tianran/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha