

Lugha Nyingine
Waathirika wa mafuriko katika Kaunti ya Lamu nchini Kenya wapokea msaada
(CRI Online) Desemba 26, 2023
Waathirika wa mafuriko wanaoishi katika Kaunti ya Lamu nchini Kenya wamepokea fedha na misaada mingine ya kibinadamu.
Kwa mujibu wa ripoti ya serikali ya Kaunti ya Lamu kuhusu janga la El-Nino, jumla ya familia 2,599 zimeathiriwa na mafuriko, ambapo familia 822 hazina makazi baada ya nyumba zao kuharibiwa na mafuriko hayo.
Kaunti ya Lamu ina karibu kambi 12 za waathirika waliohama vijijini kwao baada ya nyumba zao kusombwa na mafuriko, zikiwemo Moa, Kitumbini, Lumshi A na B, na Mikinduni B.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma