

Lugha Nyingine
Jeshi la Uganda lasema limemuua kiongozi wa waasi wa ADF kwenye mashambulizi ya hivi karibuni
Jeshi la Uganda limesema limemuua kiongozi mkuu wa kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF) waliohusika na mashambulizi ya hivi karibuni katika wilaya ya magharibi ya Kamwenge.
Katika taarifa yake msemaji wa jeshi la Uganda, Kanali Deo Akiiki, amemtaja kiongozi huyo wa tawi kuwa ni Musa Kamusi, akisema mbali na kumuua kiongozi huyo aliyekuwa akiwahangaisha raia huko Kamwenge, pia wamekamata bunduki moja ya PK na nyingine ya AK-47 iliyokuwa na risasi kadhaa.
Haya yanajiri siku moja baada ya waasi wa ADF kushambulia na kuua raia watatu wakiwemo watoto wawili huko Kamwenge. Wiki iliyopita, waasi hao hao waliua watu 10 katika wilaya moja. Jeshi limeanza mchakato wa kuajiri askari wa vitengo vya ulinzi vya ndani ili kuimarisha usalama katika eneo hilo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma