Watu wasiopungua 20 wauawa katika shambulizi la Israel dhidi ya jengo moja kusini mwa Gaza

(CRI Online) Desemba 28, 2023

Wizara ya Afya ya Gaza imesema shambulizi la mabomu lililofanywa na Israel siku ya Jumatano dhidi ya jengo moja lililoko karibu na hospitali katika mji wa Khan Younis, kusini mwa Ukanda wa Gaza limesababisha watu wasiopungua 20 kuuawa na wengine makumi kujeruhiwa.

Msemaji wa wizara hiyo Bw. Ashraf al-Qedra amesema kwenye taarifa kuwa idadi ya vifo inaweza kuongezeka wakati ambapo waokoaji wanaendelea kutafuta manusura chini ya vifusi vya jengo hilo.

Vyanzo vya ndani vya habari vimeliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa wakati shambulizi hilo lilipotokea kulikuwa na Wapalestina wengi wasio na makazi ndani ya jengo hilo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha