

Lugha Nyingine
Hafla ya Kutunukia Washindi wa Tuzo ya tatu ya “Wajumbe wa Urafiki wa Njia ya Hariri” yafanyika Beijing, China
Tarehe 27, Desemba, hafla ya kutunukia washindi wa tuzo ya tatu ya “Wajumbe wa Urafiki wa Njia ya Hariri” ilifanyika hapa Beijing, China ikifadhiliwa kwa pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Mabadilishano ya Kitamaduni cha China na Jarida la “Global People” la Gazeti la People’s Daily, na kuandaliwa kwa pamoja na Kampuni ya Kimataifa ya Utamaduni na Sanaa ya China.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya 13 ya Taifa ya Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China, ambaye pia ni Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Mabadilishano ya Kitamaduni cha China, Yang Chuantang, naibu mkuu wa Shirika la People’s Daily Hu Guo, na manaibu wakuu wa kituo hicho Li Baodong, He Jianzhong, Xu Lirong na wageni wengine waalikwa walihudhuria hafla hiyo.
Ikiwa na kaulimbiu isemayo “simulizi za wajenzi wa ‘Ukanda Mmoja, Njia Moja’”, tuzo hiyo iliteua vikundi 11 vya “wajumbe wa urafiki wa njia ya hariri” kutoka washindani zaidi ya 100 duniani. Washindi wa tuzo hiyo wanatoka nchi zaidi ya 10 za mabara ya Asia, Afrika, Ulaya, Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kusini na Oceania, wakijihusisha na nyanja mbalimbali kama vile siasa, uchumi, utamaduni, elimu na matibabu.
Mshindi Abderrahmane Salem akitoa hotuba kwa kupitia video.
Abderrahmane Salem kutoka Mauritania ni moja kati ya washidi hao. Miaka 8 iliyopita, Abderrahmane alikuwa ni msanifu wa “Ukuta Mkuu wa Kijani” wa Mauritania. Leo “ukuta imara” wa miti ya kijani unaenea katika mpaka wa kusini wa Jangwa la Sahara. Eneo hili ambalo hapo awali lilikuwa likifunikwa na dhoruba ya mchanga linageuzwa kuwa pepo ya wanyama na mimea.
“Ukuta Mkuu wa Kijani” wa Afrika unahamasishwa na “Misitu ya Kulinda Mchanga ya Maneno Matatu ya Kaskazini” ya China. Mnamo mwaka 2023, Abderrahmane alitembelea China mara mbili, ili kujifunza uzoefu bora wa kuzuia na kudhibiti hali ya kuenea kwa jangwa. Alisema kwa kusisimka, “Mafanikio ya China katika eneo hili yametushangaza sana! Ninataka kuyapeleka nyumbani Mauritania.” Njia ya ushirikiano kati ya China na Afrika katika udhibiti na uzuiaji wa jangwa imekuwa njia ya urafiki inayounganisha mioyo ya watu wa pande hizo mbili.
Kwenye sehemu ya hafla hiyo, mabalozi wanaowakilisha nchi zaidi ya 10 nchini China, na wadau zaidi ya 300 wanaofuatilia ujenzi wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” kutoka ndani na nje ya China walikusanyika na kusikiliza kwa pamoja simulizi za wajumbe wa urafiki kuhusu mabadilishano kati ya tamaduni tofauti na simulizi ya Njia ya Hariri ya urafiki wa karibu kati ya watu.
Usiku wa tuzo hiyo, miradi ya “Ushirikiano wa Kimataifa wa Afya wa Njia ya Hariri” na “Mpango wa Ujasiriamali wa Vijana wa Njia ya Hariri” ilifanya hafla za uzinduzi na utiaji saini hapo hapo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma