

Lugha Nyingine
Wizara ya Ulinzi ya China yasema mazungumzo kati ya majeshi ya China na Marekani yamepata maendeleo ya kiujenzi
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya China Bw. Wu Qian amesema mazungumzo yaliyofanyika hivi karibuni kwa njia ya video kati ya maafisa waandamizi wa majeshi ya China na Marekani yamepata maendeleo ya kiujenzi.
Akizungumza na waandishi wa habari siku ya Alhamisi Bw. Wu amesema mjumbe wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) Bw. Liu Zhenli alizungumza na Mkuu wa Wakuu wa Majeshi ya Marekani Bw. Charles Brown kupitia video tarehe 21 mwezi huu ambapo maafisa hao walibadilishana maoni kwa kina juu ya utekelezaji wa maafikiano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo mbili mjini San Francisco pamoja na masuala mengine yanayofuatiliwa kwa pamoja na pande hizo mbili.
Amesema China inatarajia kuwa Marekani itafanya juhudi pamoja na China kuhimiza uhusiano wa kijeshi kati yao kupata maendeleo thabiti katika msingi wenye na usawa na kuheshimiana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma