

Lugha Nyingine
Mradi wa umeme JNHPP nchini Tanzania wafikia asilimia 94.78
(CRI Online) Desemba 29, 2023
Naibu Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Nishati wa nchi hiyo, Dkt. Doto Biteko amesema, utekelezaji wa Mradi wa Bwawa Kuzalisha Umeme kwa Maji wa Julius Nyerere (JNHPP), utakaozalisha umeme wa megawati 2,115 kwa sasa umefikia asilimia 94.78, huku mashine mbili za kuzalisha umeme zimeshafungwa tayari kwa ajili ya kuanza kuzalisha umeme.
Dkt. Biteko amesema hayo alipofanya ziara ya kukagua mradi huo wilayani Rufiji. Amesema, itakapofika Jumanne wiki ijayo, majaribio ya kwanza yatakuwa yamekamilika na itakapofika Februari 19 mwakani, majaribo ya pili yatakuwa yamekamilika tayari kwa kuanza kuzalisha umeme.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma