Rais Xi asema kuimarisha na kuendeleza kwa siku zote uhusiano kati ya China na Russia kunasaidia maslahi ya kimsingi ya nchi zote mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 02, 2024

BEIJING - Maendeleo ya uhusiano kati ya China na Russia katika miaka 75 iliyopita umeonyesha kuwa kuimarisha na kuendeleza kwa siku zote uhusiano wa pande hizo mbili wenye urafiki wa kudumu na ujirani mwema, uratibu wa kimkakati wa pande zote na ushirikiano wa kunufaishana kunasaidia maslahi ya kimsingi ya nchi hizo mbili, Rais Xi Jinping wa China amesema siku ya Jumapili alipotumiana ujumbe wa salamu za Mwaka Mpya na mwenzake wa Russia, Vladimir Putin.

Kwa niaba ya serikali na wananchi wa China, Rais Xi ametoa pongezi za dhati na salamu za heri kwa Rais Putin na watu wa Russia.

Amesema, licha ya mabadiliko ambayo hayaonekana katika miaka 100 iliyopita na hali tete ya kimataifa na kikanda, uhusiano kati ya China na Russia daima umedumisha maendeleo imara na tulivu, na kusonga mbele katika mwelekeo sahihi Mwaka 2023.

Chini ya mwongozo wa pamoja wa viongozi hao wawili, pande hizo mbili zimeimarisha zaidi hali ya kuaminiana kisiasa, kuimarisha uratibu wa kimkakati na kupata matokeo mapya katika ushirikiano wa kunufaishana, Rais Xi amesema.

Amesema yeye na Rais Putin kwa pamoja wametangaza kuwa pande hizo mbili zitaadhimisha Miaka ya Utamaduni kati ya China na Russia Mwaka 2024-2025, huku akibainisha kuwa nchi hizo pia zitaadhimisha miaka 75 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Russia.

Rais Xi amesema yuko tayari kudumisha mawasiliano ya karibu na Rais Putin, na anatarajia kutumia shughuli hizo kama fursa ya kuziongoza nchi hizo mbili ili kuongeza hali ya kuaminiana, kupanua ushirikiano na kuendeleza urafiki ili kuhakikisha kuwa uhusiano kati ya China na Russia unaendelea kwa kasi katika njia sahihi.

Katika ujumbe wake, Rais Putin ametoa salamu za dhati za Mwaka Mpya kwa Rais Xi na kuwatakia watu wa China furaha na afya njema.

Ameeleza kuwa walikutana mara mbili mwaka huu, na kutia msukumo mkubwa katika maendeleo ya pande zote ya uhusiano na ushirikiano wa uratibu wa kimkakati katika pande zote wa zama mpya kati ya Russia na China.

Ameongeza kuwa, inaaminika kuwa kwa juhudi za pamoja za pande zote mbili, ushirikiano wenye matokeo mengi kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali utaleta mafanyikio makubwa zaidi na ushirikiano wa pande mbili ndani ya mifumo ya Umoja wa Mataifa, G20, Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai na BRICS pia utapata maendeleo mapya.

Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu wa China Li Qiang na Waziri Mkuu wa Russia Mikhail Mishustin walitumiana salamu za Mwaka Mpya.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha