Safari za abiria nchini China zaongezeka wakati wa likizo ya Mwaka Mpya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 02, 2024

Abiria wanapita lango la kutokea la kituo cha treni cha Nanjing Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Januari 1, 2024. (Picha na Su Yang/Xinhua)

Abiria wanapita lango la kutokea la kituo cha treni cha Nanjing Mkoa wa Jiangsu, Mashariki mwa China, Januari 1, 2024. (Picha na Su Yang/Xinhua)

BEIJING - Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ya China imekadiria jana Jumatatu kuwa, Idadi ya abiria waliohudumiwa kupitia mtandao wa usafiri wa China wakati wa likizo ya Mwaka Mpya imekadiriwa kufikia zaidi ya milioni 128, ikiwa ni ongezeko la asilimia 78.4 kuliko ile ya mwaka uliopita.

Takwimu zilizotolewa na wizara hiyo zimeonesha kuwa, Wakati wa likizo hiyo ya siku tatu ya Mwaka Mpya iliyomalizika Jumatatu, mtandao wa reli wa China ulikuwa ukikadiriwa kushuhudia safari za abiria milioni 44.2, ikiongezeka kwa asilimia 177.5 kuliko zile za kipindi kama hicho cha likizo mwaka mmoja uliopita.

Wizara hiyo imesema, Kuanzia Jumamosi hadi Jumatatu, mtiririko wa abiria kwa usafiri wa ndege ulikuwa ukikadiriwa kufikia milioni 5.19, ikiongezeka kwa asilimia 140.3 zaidi kuliko mwaka jana, huku takwimu za barabara kuu na njia za majini zikitarajiwa kuongezeka kwa asilimia 46.1 na asilimia 72.9, mtawalia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha