China yazitaka nchi husika kuheshimu ipasavyo ukweli kwamba Hong Kong tayari imerejea China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2024

BEIJING - Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin siku ya Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari alipoulizwa kuhusu taarifa inayohusika na Hong Kong iliyotolewa hivi karibuni na nchi zikiwemo Uingereza na Marekani kwa jina la "Muungano wa Uhuru wa Vyombo vya Habari" alizitaka nchi husika kuheshimu ipasavyo ukweli kwamba Hong Kong tayari imerejea China na kuacha mawazo yao ya kikoloni.

Huku akieleza kuwa hii ni kupaka matope uhuru wa vyombo vya habari mkoani Hong Kong, ni shambulio dhidi ya utekelezaji wa sheria halali ya Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong (HKSAR), na ni kitendo cha kuwatia moyo Jimmy Lai na watu wanaoipinga China na wanaohusika katika kuivuruga Hong Kong. Wang amesema China inasikitishwa na kupinga kwa uthabiti kile kinachoitwa kauli kutoka kwa nchi chache kwa jina la "Muungano wa Uhuru wa Vyombo vya Habari".

Kesi za Julian Assange na Edward Snowden tayari zimeonyesha Dunia kwamba kile kinachoitwa "uhuru wa vyombo vya habari" ni chombo tu ambacho kinatumiwa na baadhi ya nchi kushambulia na kupaka matope wengine, Wang amesema.

"Nchi hizi hazijali sana uhuru wa vyombo vya habari wakati maslahi yao ya kibinafsi yanapohusika. Wametoa kauli zisizowajibika juu ya mambo yanayoihusu Hong Kong kwa jina la uhuru wa vyombo vya habari kwa sababu tu hawafurahii ustawi wa Hong Kong, na bado wanatumai kudumisha mapendeleo na ushawishi wao wa zamani huko Hong Kong lakini hawawezi kufanikiwa," Wang amesema.

Wang amesema Hong Kong inafuata utawala kwa mujibu wa sheria, na sheria zote za Hong Kong lazima zitiliwe maanani na wale wanaovunja sheria lazima wawajibishwe na kwamba tangu Sheria ya Usalama wa Taifa ilipoanza kutumika Hong Kong, mkoa huo umerejesha utulivu na uko katika hali ya kustawi.

"Jaribio lolote la kuingilia masuala ya Hong Kong kwa jina la uhuru wa vyombo vya habari haliwezi kufanikiwa," amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha