Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao nchini China lakaribisha abiria zaidi ya milioni 16 Mwaka 2023

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 03, 2024

Kundi la kwanza la watalii wanaotembelea kisiwa kilichojengwa na binadamu  cha mashariki cha Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao  wakipiga picha pamoja Desemba 15, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

Kundi la kwanza la watalii wanaotembelea kisiwa kilichojengwa na binadamu cha mashariki cha Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao wakipiga picha pamoja Desemba 15, 2023. (Xinhua/Liu Dawei)

GUANGZHOU - Katika Mwaka 2023, abiria wa kuingia na kutoka zaidi ya milioni 16.3 na magari milioni 3.26 yalipita Bandari ya Zhuhai ya Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao (HZMB) la China, ambalo ni kivuko kirefu zaidi cha daraja-na-handaki duniani, ikiwa ni mara 1.29 na mara 3.8 zaidi ya Mwaka 2019, mtawaliwa, takwimu rasmi zinaonyesha, huku makundi ya watalii yakiongoza mtiririko mkuu wa watalii wanaopita daraja hilo.

Takwimu zilizotolewa siku ya Jumanne na kituo cha ukaguzi cha mpaka cha daraja hilo zimeonesha kuwa, Mwaka 2023, makundi zaidi ya 45,000 ya watalii wa China Bara yalisafiri kwenda na kutoka Mikoa ya Utawala Maalum ya Hong Kong na Macao ya China kupitia daraja hilo. Wakati huo huo, wakazi wa Hong Kong na Macao walifanya safari zilizovunja rekodi ya juu zaidi zinazokadiriwa kufika karibu milioni 10 za kutembelea China Bara kupitia daraja hilo.

Mfanyakazi wa kituo hicho amesema kuwa, Mwaka 2023, mtiririko wa juu zaidi wa abiria kwa siku moja kupitia daraja hilo ulifikia 115,000, na kufikia rekodi mpya ya juu tangu daraja hilo lilipoanza kufanya kazi.

Daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macao (HZMB) lenye urefu wa kilomita 55 linaunganisha Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong wa China, Mji wa Zhuhai katika Mkoa wa Guangdong wa Kusini mwa China, na Mkoa wa Utawala Maalum wa Macao wa China. Limeleta fursa na manufaa makubwa katika Eneo la Ghuba Kuu ya Guangdong-Hong Kong-Macao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha