

Lugha Nyingine
Wizara ya Mambo ya Nje ya China yazungumzia maadhimisho ya miaka 45 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani
China na Marekani mwaka huu zinaadhimisha kutimia miaka 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, ambapo siku ya Jumatatu, Rais Xi Jinping wa China na mwenzake Joe Biden walitumiana salamu za pongezi kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Ikizungumzia maadhimisho hayo, wizara ya mambo ya nje ya China imesema siku ya Jumanne kuwa kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Marekani ni tukio muhimu katika historia ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na uhusiano wa kimataifa na kwamba kwa miaka 45, uhusiano kati ya China na Marekani umekabiliana na changamoto na mafanikio mengi hadi kufika hapa ulipo sasa.
Kuhusu biashara baina ya nchi mbili, wizara hiyo imesema ilipanda kutoka chini ya dola bilioni 2.5 mwaka 1979 hadi kufikia dola bilioni 760 mwaka 2022, ambapo uwekezaji wa pande mbili uliongezeka kutoka karibu sifuri hadi zaidi ya dola bilioni 260. Nchi hizo mbili pia zimefanya ushirikiano muhimu katika maeneo muhimu ya kimataifa na kikanda na masuala ya kimataifa.
Wizara hiyo pia imebainisha kuwa historia inaonesha kukua kwa uhusiano kati ya China na Marekani siyo tu kunachangia manufaa ya watu wa nchi hizo mbili bali pia amani, utulivu na maendeleo ya dunia.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma