

Lugha Nyingine
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China atoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kukabiliana pamoja na mgawanyiko wa kiuchumi
BEIJING - Jumuiya ya kimataifa inahitaji kufanya juhudi za pamoja na kuungana mkono katika kukabiliana na msukosuko wa kiuchumi uliopo na kufanya kazi kwa ajili ya mustakabali mzuri wa siku za baadaye wa Dunia, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Wang Wenbin amesema siku ya Jumatano.
Iliripotiwa kuwa katika mahojiano ya Januari 2, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) Kristalina Georgieva alionya kuwa, kugawanyika kwa uchumi wa Dunia kwa kufuata misingi ya siasa za kijiografia kutokana na kuongezeka kwa vizuizi vya usalama wa kitaifa, kumezifanya nchi zikigawanyika katika kambi tofauti zinazoongozwa na Marekani na China. Alisema, kama uwepo wa hali hii utaendelea, hatimaye utasababisha Pato la Dunia (GDP) kupungua kwa asilimia 7.
Alipoulizwa maoni kuhusu ripoti husika, Wang ameuambia mkutano na waandishi wa habari kwamba kuna sayari moja tu tunayoiita nyumbani, na binadamu wana mustakabali mmoja wa pamoja.
"Kinachohitajika zaidi ni mshikamano, na kinachopaswa kuepukwa zaidi ni kugawanyika," amesema.
Wang amesema vita vya kibiashara, vita vya kiteknolojia, au kutengana kiuchumi, kukata minyororo ya viwanda na usambazaji, na kuondoa hatari za kiuchumi, vyote hivi vimesanifiwa kimsingi kuingiza siasa katika masuala ya biashara na kutumika kama silaha ili kudumisha ukuu wa nchi fulani, kurudisha nyuma nchi zinazojitokeza kwenye masoko na kuzuia juhudi za nchi zinazoendelea katika njia zao za kujipatia maendeleo, na kuwanyima watu bilioni 7 haki ya maisha bora.
"Hili si jambo zuri na si la endelevu. Hatimaye, ni maslahi ya jumla ya jumuiya ya kimataifa yatakayoathirika na hakuna nchi moja inayoweza kuepushwa," amesema Wang.
Msemaji huyo amesema, Dunia haitarudi nyuma kwa hali ya kutengana na kuwekwa katika upekee wa nchi fulani, China ingependa kushirikiana na pande zote ili kutetea utandawazi wa kiuchumi wenye manufaa na ulio shirikishi kwa wote na kukataa kithabiti hali ya kuondoa utandawazi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma