Bandari ya Dalian, China yazindua njia ya meli ya kontena kwenda Amerika Kusini

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2024

Picha hii iliyopigwa Januari 2, 2024 ikionyesha meli ya kontena iitwayo "WAN HAI 357" ikitia nanga kwenye Bandari ya Dalian Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China. (Kampuni ya Bandari ya Liaoning / Xinhua)

DALIAN - Meli ya kontena, iitwayo "WAN HAI 357," iliyopakia makontena 3,000 ya TEU ya bidhaa, kama vile ndizi na samaki kamba weupe ambayo iliondoka Bandari ya Guayaquil nchini Ecuador Desemba 28 imewasili kwenye Bandari ya Dalian katika Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China siku ya Jumanne, ikiashiria njia ya kawaida ya meli za kontena inayounganisha bandari hiyo na pwani ya magharibi ya Amerika Kusini imezinduliwa rasmi.

Njia hiyo inaunganisha Bandari ya Dalian na bandari za nchini Colombia na Ecuador pamoja na bandari nyingine kuu kwenye pwani ya magharibi ya Amerika Kusini. Safari nzima sasa inachukua siku 25 pekee, ikipunguza angalau siku saba ikilinganishwa na hali ya awali ya usafirishaji kupitia vituo vingine. Hii itaharakisha kuingia kwa bidhaa zinazosafirishwa kwa mnyororo baridi, kama vile vyakula vya baharini na matunda, kutoka Amerika Kusini hadi soko la kaskazini mashariki mwa China.

Njia hiyo mpya inaendeshwa mara moja kwa wiki na Kampuni ya Uchukuzi ya WAN HAI LINES ya Taiwan, ambayo ina meli sita za kubeba kontena 3,000 ya TEU.

Kwa mujibu wa Li Xiaoguang, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Bandari ya Kontena ya Dalian ya Kundi la Kampuni za Bandari ya Liaoning, ambayo inasimamia bandari ya Dalian, kwa sasa kuna njia 105 za meli za kontena kutoka Bandari ya Dalian, zikifika kwenye bandari zaidi ya 300 katika nchi na maeneo zaidi ya 160 kote duniani.

Picha hii iliyopigwa Januari 2, 2024 ikionyesha kontena likipakiwa kwenye meli ya kontena iitwayo "WAN HAI 357" katika Bandari ya Dalian, Mkoa wa Liaoning, Kaskazini Mashariki mwa China. (Kampuni ya Bandari ya Liaoning / Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha