Uzuri wa majira ya baridi wa China wavutia watu wa Malta

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2024

Picha hii ikionyesha watalii wakitembelea Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin mkoani Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China, Desemba 31, 2023. (Xinhua/Zhang Tao)

Picha hii ikionyesha watalii wakitembelea Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin mkoani Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China, Desemba 31, 2023. (Xinhua/Zhang Tao)

VALLETTA - Picha za mandhari ya kuvutia ya barafu na theluji ya China, zilizochapishwa na Kituo cha Utamaduni cha China nchini Malta, zimezua shauku na kupendwa sana na watu wa Malta.

"Sijawahi kuona mvuto ulioje wa majira ya baridi nchini China," mwandishi wa Malta Fiona Vella amesema baada ya kufuatilia shughuli za utalii za majira ya baridi ya China kwa kupitia maelezo, video, picha na makala zilitolewa na kituo hicho.

"Hewa yenye ubaridi, iliyopambwa na chembe za theluji maridadi, imebadilisha mandhari nzuri kuwa mandhari ya ajabu, ikiweka maajabu kwenye maeneo ya kale na mandhari ya miji ya kisasa vile vile," ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

Vella amewahi kutembelea China mara kadhaa na amevutiwa sana na mandhari nzuri ya mazingira asili ya China, historia ndefu na utamaduni tajiri. Kufahamishwa kuhusu mila na desturi za kale ambazo bado zinafuatwa na watu, kwa mfano, kuvua samaki katika majira ya baridi katika Ziwa Chagan mjini Songyuan, Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China, kumemwacha kumbukumbu nyingi, amesema.

Watu wakitembelea Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin  mkoani Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China, Januari 1, 2024. (Xinhua/Xie Jianfei)

Watu wakitembelea Bustani ya Barafu na Theluji ya Harbin mkoani Heilongjiang, Kaskazini Mashariki mwa China, Januari 1, 2024. (Xinhua/Xie Jianfei)

"Sasa ninatamani kutembelea maeneo mbalimbali ya China, kuanzia sherehe za majira ya baridi kali hadi mandhari tulivu, kuufahamu utamaduni tajiri wa China katika msimu huu wa kipekee na wa kuvutia," Vella amesema.

Baada ya mafanikio ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing 2022, sekta ya utalii wa barafu na theluji nchini China imeshuhudia ukuaji mkubwa. Wachina zaidi wanaonyesha kupendezwa na michezo ya majira ya baridi, na watalii wa kigeni wanachagua China kwa safari zao za majira ya baridi.

Huku maeneo ya mapumziko ya majira ya baridi nchini China sasa yakifunguliwa kwa umma, watalii wa kimataifa pia wanaalikwa kufurahia mandhari ya China katika majira ya baridi kali.

Hafla ya ufunguzi wa tamasha la uvuvi wa majira ya baridi kali ikifanyika kwenye Ziwa Chagan katika Mji wa Songyuan, Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China, Desemba 28, 2023.(Xinhua/Zhang Nan)

Hafla ya ufunguzi wa tamasha la uvuvi wa majira ya baridi kali ikifanyika kwenye Ziwa Chagan katika Mji wa Songyuan, Mkoa wa Jilin, Kaskazini Mashariki mwa China, Desemba 28, 2023.(Xinhua/Zhang Nan)

Mtelezi akifurahia kuteleza kwenye theluji  katika eneo la V-PARK la Mji wa Jilin, Mkoa wa Jilin, Kaskazini-Mashariki mwa China, Februari 11, 2023.(Xinhua/Tao Xiyi)

Mtelezi akifurahia kuteleza kwenye theluji katika eneo la V-PARK la Mji wa Jilin, Mkoa wa Jilin, Kaskazini-Mashariki mwa China, Februari 11, 2023.(Xinhua/Tao Xiyi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha