Msanii wa Uganda aunganisha ubora wa kauri za China na sanaa za Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 04, 2024

Robert anayetoka Uganda sasa anasoma shahada ya uzamivu ya somo la usanifu katika Chuo Kikuu cha Kauri cha Jingdezhen. Kabla ya kusoma katika Chuo Kikuu, amevutiwa sana na ustadi wa kutengeneza vyombo vya kauri, na katika wakati wa kusoma kozi yake ya ustadi wa China wa kutengeneza vyombo vya kauri, amepata uelewa mzuri wa kuunganisha ubora wa Afrika na ubora wa China katika kazi yake ya kutengeneza vyombo vya kauri, na kuunda mtindo wake wa kipekee.

Hivi karibuni kijana huyo wa Uganda atafanya maonyesho yake binafsi ya vyombo vya kauri yanayoitwa "Umoja wa Vitu Tofauti," maana yake ni kuunganisha utamaduni wa aina tofauti kuwa umoja wa tamaduni, umaalumu huo wa kazi yake ya kutengeneza vyombo vya kauri ndio anaojivunia zaidi.

Amekaza nia ya kuendeleza kazi yake yenye umaalumu huo katika maskani yake Uganda siku za baadaye, pia ameamini kuwa, kwa kupitia kazi yake ataweza kujenga daraja la kuwawezesha watu wengi waelewe mvuto wa vyombo vya kauri vya China na kukuza zaidi mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha