Israel yasema Wapalestina wataongoza masuala ya kiraia Ukanda wa Gaza baada ya mapambano kumalizika

(CRI Online) Januari 05, 2024

Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant amesema jana Alhamisi kuwa, Wapalestina wataongoza masuala ya kiraia katika Ukanda wa Gaza, huku Israel ikidumisha udhibiti wa usalama wa eneo hilo baada ya mapigano ya sasa na Kundi la Hamas kumalizika.

Bw. Gallant amesema, hakutakuwa na raia wa Israel katika ukanda wa Gaza baada ya malengo ya vita ya sasa kutimizwa, na pia amesisitiza kuwa Israel haitaruhusu kundi la Hamas kutawala Gaza au kuhatarisha usalama wa waisraeli, kwa hivyo itabaki na uhuru wa kuchukua hatua huko Gaza.

Waziri huyo amesema Israel inaingia kwenye kile alichokiita kipindi cha tatu cha mapigano, ambacho kitahusisha mashambulizi, uharibifu wa mahandaki ya magaidi, shughuli za angani na ardhini, na operesheni maalumu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha