

Lugha Nyingine
Rais wa Zanzibar aipongeza China kwa kujenga makazi kwa ajili ya matabibu
(CRI Online) Januari 05, 2024
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi nchini Tanzania Dr. Hussein Ali Mwinyi ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa eneo la makazi kwa ajili ya matabibu katika hospitali ya Abdulla Mzee kisiwani Pemba siku ya Jumatano.
Rais Mwinyi amesema makazi hayo yanayojengwa na Kundi la Kampuni za Zhengtai kutoka Mkoa wa Jiangsu wa China yatasaidia wafanyakazi wa hospitali hiyo wanaoishi mbali na kituo chao cha kazi.
Rais Mwinyi ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa makazi hayo, ikiwa ni sehemu ya shughuli za kumbukumbu kabla ya maadhimisho ya kutimia miaka 60 tangu kutokea kwa mapinduzi ya Zanzibar, yaliyotokea Januari 12, mwaka 1964.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma