Watu milioni 1.5 wahitaji msaada wa kibinadamu nchini Kenya

(CRI Online) Januari 05, 2024

Mamlaka ya Taifa ya Kukabiliana na Ukame nchini Kenya (NDMA) imesema, watu milioni 1.5 nchini humo wanahitaji msaada wa kibinadamu, huku wengi wao ni wale waliokumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za EI Nino za hivi karibuni.

NDMA imesema siku ya Alhamisi kwamba, tathmini kuhusu athari ya msimu mrefu wa mvua wa mwaka 2023 kwa chakula na usalama wa lishe, inakadiria kuwa idadi ya watu wanaohitaji msaada wa kibinadamu kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2023 hadi mwezi Januari mwaka huu itapungua na kufikia milioni 1.5 kutoka milioni 2.8 ya mwezi Julai mwaka 2023.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha