

Lugha Nyingine
Wanafunzi zaidi ya milioni 10 kunufaika na mradi wa maktaba ya mtandao Tanzania
Wanafunzi zaidi ya milioni 11 na walimu zaidi ya laki 2 katika shule za umma za Tanzania watanufaika na mradi mpya wa maktaba ya mtandao nchini humo.
Mradi huo umeratibiwa na Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE) kwa kushirikiana na kampuni ya Snapplify yenye makao makuu nchini Afrika Kusini inayojishughulisha na teknolojia ya elimu.
Ofisa Uhusiano wa kampuni ya Snapplify, Stephen Bestbier amewaambia wanahabari mjini Dar es Salaam, Tanzania kuwa mradi huo unalenga kuleta mabadiliko kwenye sekta ya elimu kwa kuwezesha upatikanaji wa raslimali za elimu bora kote nchini, akiongeza kuwa mradi huo ni miongoni mwa miradi mikubwa zaidi ya elimu ya kidijitali katika Bara la Afrika. Mradi huo utanufaisha shule zaidi ya 19,000 za serikali ndani ya miaka mitatu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma