

Lugha Nyingine
Wachimbaji madini 15 walionaswa mgodini nchini Zimbabwe waokolewa
(CRI Online) Januari 08, 2024
Ripoti ya Gazeti la Herald la Zimbabwe imesema wachimbaji madini 15 walionaswa mgodini wameokolewa jana Jumapili kufuatia kuporomoka kwa mgodi mmoja wa dhahabu nchini humo.
Wachimbaji hao walinaswa asubuhi ya Alhamisi ya wiki iliyopita wakati mgodi wa Redwing huko Penholonga, umbali wa kilomita 265 kutoka mji wa Harare, uliporomoka kutokana na kinachohisiwa kuwa ni tetemeko la ardhi.
Baadaye teknolojia ya setilaiti ilitumiwa kuhakikisha mahali wachimbaji madini hao walipo na shimo likatobolewa kuweka njia ya kuwatoa.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma