Wanajeshi waua wanamgambo 76 wa al-Shabaab katikati mwa Somalia

(CRI Online) Januari 08, 2024

Maofisa wa Somalia wamesema jeshi la taifa la Somalia (SNA) likiungwa mkono na washirika wa kimataifa limeua wanamgambo 76 wa kundi la al-Shabaab na kujeruhi kadhaa kufuatia operesheni ya siku mbili katika eneo la Mudug katikati mwa Somalia.

Mkuu wa jeshi la Somalia Bw. Ibrahim Sheikh Muhidin amesema makamanda wakuu wa kundi la al-Shabaab ni miongoni mwa watu waliouawa wakati wa mashambulizi hayo yaliyofanyika Jumamosi na mapema Jumapili.

Ameongeza kuwa mashambulizi hayo pia yameharibu kambi na magari ya al-Shabaab, na wanajeshi walikuwa wanapiga hatua katika kutokomeza wanamgambo hao kutoka kwenye ngome zao katikati na kusini mwa Somalia.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha