Rais wa Somalia afuta makubaliano ya bandari kati ya Ethiopia na Somaliland

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 08, 2024

MOGADISHU - Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amebatilisha makubaliano yaliyofikiwa kati ya Ethiopia na Somaliland ambayo yangeifanya Addis Ababa ipate ufikiaji wa bandari kwa mabadilishano ya kutambulia Hargeisa, mji mkubwa zaidi wa Somaliland.

Rais Mohamud alisema siku ya Jumamosi kwamba ametia saini na kuidhinisha muswada wa sheria uliopitishwa na mabaraza mawili ya bunge la nchi hiyo wa kubatilisha "Mkataba haramu wa Maelewano" ambao ulitiwa saini Januari 1 ili kuipa Ethiopia isiyo na ufikiaji wa bahari haki ya kutumia bandari ya Bahari Nyekundu ya Berbera, hatua ambayo Mogadishu iliiita kuwa ni ukiukaji wa mamlaka na ukamilifu wa ardhi yake na kutoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuingilia kati.

Rais huyo amesema katika taarifa iliyotolewa mjini Mogadishu, kwamba hatua hiyo inadhihirisha dhamira ya kudumisha umoja, mamlaka na ukamilifu wa ardhi.

"Kwa kuungwa mkono na wabunge wetu na watu wetu, sheria hii ni kielelezo cha dhamira yetu ya kulinda umoja, mamlaka na ukamilifu wa ardhi yetu kwa kuendana na sheria za kimataifa," rais huyo amesema.

Rais Mohamud, ambaye serikali yake imemwita nyumbani balozi wake kutoka Ethiopia, amesisitiza kuwa sheria hii inawakilisha msimamo rasmi wa Mogadishu kuhusu makubaliano hayo na inafanya kazi kama kizuizi kikubwa dhidi ya uvamizi wowote katika ardhi ya Somalia.

Makubaliano hayo, ambayo yanairuhusu Ethiopia kuanzisha shughuli za kibiashara za baharini na kufikia kituo cha kijeshi kilichokodishwa kwenye Bahari Nyekundu, yamelaaniwa na serikali ya Somalia, Wasomali kote duniani zikiwemo nchi za kigeni ambazo zimeitaja hatua hiyo kuwa "kitendo cha uchokozi" .

Chini ya makubaliano hayo, Somaliland, ambayo ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia Mwaka 1991 na haijatambuliwa kimataifa, ingetambuliwa na Ethiopia na kupokea sehemu ya hisa za shirika la ndege la Ethiopia linalomilikiwa na serikali.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha