Kambi ya mafunzo ya michezo yakuza vipaji vya vijana nchini Namibia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 08, 2024
Kambi ya mafunzo ya michezo yakuza vipaji vya vijana nchini Namibia
Watoto wakishiriki katika kambi ya mazoezi ya michezo pamoja na makocha wao mjini Windhoek, Namibia, Januari 6, 2023. (Picha na Ndalimpinga Iita/ Xinhua)

WINDHOEK - Namibia ilifanya Kambi ya 31 ya kila mwaka ya Ukocha na Mafunzo ya Quinton-Steele Botes (QSB) wiki iliyopita katika mji mkuu, Windhoek ili kukuza vipaji vya vijana na kuongeza shauku ya michezo ambapo kambi hiyo iliyofanyika Januari 3 hadi 6, ilianzishwa Mwaka 1993 na Quinton-Steele Botes, msimamizi mashuhuri wa michezo wa Namibia ambaye aliaga dunia Mwaka 2014.

Mafunzo hayo yalilenga zaidi mbinu za mbinu za michezo kama vile kurusha, kukimbia kwa kasi mbio fupi, kuruka viunzi na kuruka juu wima na kwa ulalo, yakiwezeshwa na makocha kutoka Namibia, Afrika Kusini, na Uholanzi.

Leoni van Rensburg, mratibu wa kambi hiyo, amesema kuwa lengo lao ni kutoa mafunzo ya kitaaluma ya michezo kwa vijana wa Namibia, kukabiliana na ufinyu wa fursa hizo nchini humo, na kutumia michezo kwa ajili ya kuwezesha jamii.

"Kambi hii inaendelea kuheshimu urithi wake na kujitolea kuiweka michezo kuwa hai nchini Namibia huku ikitoa fursa kwa wale wasiojiweza," van Rensburg amesema Jumamosi.

Mwaka huu, kambi hiyo ilivutia washiriki wapatao 200, waliokusanyika katika vikundi vya programu za michezo ya watoto, vijana wa umri wa kati na wa juu.

Pia ilijumuisha kipindi maalum kwa wanaotaka kuwa makocha, kuwasaidia kuhama kutoka kuwa wasio wajuzi hadi kufundisha michezo kitaaluma, kutoa ushauri, na kuwa jukwaa la kuwasiliana.

Charley Strohmenger, kocha mashuhuri wa kuruka kwa mshazari kutoka Afrika Kusini, amezungumzia matokeo chanya ya kambi hiyo, kutoa ushauri na kutumika kama jukwaa mawasiliano.

"Nimeshiriki katika kambi hii ya QSB kwa zaidi ya miaka 21 na nimeona matokeo mazuri kutoka kwa wachezaji ambao wamefanikiwa katika michezo na wachezaji ambao wamekuwa makocha wenye leseni," Strohmenger ameeleza.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha