Rais Xi Jinping asisitiza kushinda mapambano magumu ya muda mrefu dhidi ya ufisadi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 09, 2024

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) akihutubia Mkutano wa Tatu wa Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC  Januari 8, 2024. (Xinhua/Ju Peng)

BEIJING - Xi Jinping, Rais wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) Jumatatu wakati akihutubia Mkutano wa Tatu wa Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya Chama cha CPC akitoa wito wa kuhimiza kazi ya chama ya kujifanyia mageuzi na kushinda mapambano magumu ya muda mrefu dhidi ya ufisadi.

Baada ya kufanya juhudi zisizolegalega za kupambana na ufisadi katika miaka 10 ya zama mpya, ushindi mkubwa umepatikana katika mapambano dhidi ya ufisadi, huku mafanikio hayo yakiimarishwa vya kutosha , Rais Xi amesema.

"Lakini hali bado ni mbaya na ngumu, tunapaswa kufahamu ipasavyo maendeleo mapya katika mapambano dhidi ya ufisadi na mazalia na mazingira ya rushwa," Rais Xi amesema, huku akiongeza kuwa, ni lazima kuhimiza juhudi zaidi za kushinda mapambano hayo magumu ya muda mrefu.

Rais Xi ameeleza kuwa Mwaka 2023 ni mwaka wa kwanza wa kutekeleza kwa pande zote misingi na malengo ya Mkutano Mkuu wa 20 wa CPC.

Amesema Kamati Kuu ya Chama imesukuma mbele kithabiti kazi ya chama ya kujifanyia mageuzi na kuongeza juhudi zake za kuhimiza Chama kujiendesha kwa nidhamu kali kwa pande zote, hali ambayo imehakikisha kwamba safari mpya inaanza vizuri.

Rais ametoa wito wa kuchukua hatua za uratibu ili kuhakikisha kuwa maofisa viongozi hawana ujasiri, fursa au tamaa za kuwa mafisadi, pamoja na kufanya juhudi zisizolegalega za kupanua wigo na maeneo ya kampeni za kupambana na ufisadi, na kuchukua hatua za kila baada ya muda uliowekwa na za muda mrefu za kuzuia na kudhibiti ufisadi.

Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China akihutubia Mkutano wa Tatu wa Wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC Januari 8, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

Li Xi, mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama ambaye pia ni Katibu wa Kamati Kuu ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC, akitoa ripoti ya kazi kwa niaba ya Kamati Kuu ya Ukagzi wa Nidhamu kwenye Mkutano wa Tatu wa wajumbe wote wa Kamati Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhani ya Chama cha CPC mjini Beijing, China, Januari 8, 2024. (Xinhua/Pang Xinglei)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha