Jeshi la Israel laanza awamu mpya isiyo na makali makubwa katika operesheni huko Gaza

(CRI Online) Januari 09, 2024

Msemaji wa Jeshi la Israel (IDF) Bw. Daniel Hagari amesema, jeshi hilo limeanza awamu mpya isiyo na makali makubwa katika operesheni yake ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas huko Gaza.

Amesemaa IDF sasa inageukia “kufanya mashambulizi ya mara moja moja badala ya kudumisha mashambulizi makubwa”, huku akiongeza kuwa vita imebadilika.

Bw. Hagari ameongeza kuwa Jeshi la Israel litatilia maanani mapigano dhidi ya kundi la Hamas katikati na kusini mwa Gaza, hasa karibu na miji ya Khan Younis na Deir al-Balah, huku likipunguza vikosi vyake huko Gaza.

Habari nyingine zinasema jeshi la Israel limetangaza kuwa limemuua ofisa wa kundi la Hamas, Hassan Akasha aliyeongoza mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel, katika shambulizi lake kwenye wilaya ya Beit Jann, kusini mwa Syria.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha