

Lugha Nyingine
OCHA: Usambazaji wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan unakumbwa na changamoto mbalimbali
(CRI Online) Januari 09, 2024
Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika maeneo mengi nchini Sudan umekumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kukosekana kwa usalama na ukosefu wa pesa taslimu, uporaji, urasimu, mawasiliano duni ya mtandao wa intaneti na simu na ukosefu wa wafanyakazi wa kibinadamu na kiufundi.
Pia OCHA imeongeza kuwa ukosefu wa nishati pia umeleta taabu kwa kazi hiyo ya usambazaji misaada pamoja na uzalishaji wa umeme kwa ajili ya uhifadhi wa mnyororo baridi na usambazaji wa maji.
Licha ya hayo OCHA imesema hadi kufikia Januari 4 mwaka huu, mpango wa misaada ya kibinadamu wa 2023 kwa Sudan uliorekebishwa ulikuwa umefadhiliwa kwa asilimia 40.8 tu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma