

Lugha Nyingine
Idadi ya waliofariki kutokana na kipindupindu nchini Zambia yaongezeka hadi 222
(CRI Online) Januari 09, 2024
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na wizara ya afya ya Zambia, zinaonesha kuwa idadi ya watu waliofariki kutokana na mlipuko wa kipindupindu nchini humo imeongezeka hadi 222, huku watu 5,462 wakiwa wamesha ambukizwa tangu kuzuka kwa mlipuko huo Oktoba mwaka jana.
Takwimu zilizotolewa Jumapili na wizara hiyo zinaonyesha kuwa watu 27 wamekufa na wengine 567 wameambukizwa katika kipindi cha muda wa saa 24 zilizopita.
Wizara hiyo pia imesema watu 340 wamepona na kuruhusiwa kutoka hospitalini katika kipindi hicho, na kwa ujumla idadi ya watu waliopona imefikia 4,172, wakati idadi ya watu walioko hospitalini inafikia 1,059.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma