

Lugha Nyingine
UN yalaani mauaji ya raia 28 katika tukio la uvamizi wa mifugo nchini Sudan Kusini
(CRI Online) Januari 09, 2024
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) umelaani ghasia zilizosababisha vifo vya raia 28 wiki iliyopita katika Kaunti ya Duk ya Jimbo la Jonglei.
Mamlaka ya Jimbo la Jonglei nchini humo imehusisha shambulio hilo ambalo pia limesababisha watu takriban 19 kujeruhiwa, na vijana wa kabila la Murle waliokuwa na silaha kutoka eneo jirani la Utawala la Greater Pibor.
UNMISS imetoa wito kwa pande zote zinazohusika kusitisha mashambulizi ya kulipiza kisasi, na kutumia njia za amani kutatua malalamiko yao.
Ujumbe huo pia umeitaka serikali ya Jimbo la Jonglei na mamlaka ya eneo la Utawala la Greater Pibor kufanya mazungumzo na kuwafikisha wahusika mbele ya vyombo vya sheria, na kuzuia unyanyasaji.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma