Ushirikiano wa elimu ya kazi za ufundi kati ya China na Afrika wasaidia maendeleo ya viwanda ya Afrika

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 10, 2024

 Mashindano ya Ustadi wa Kazi za Ufundi barani Afrika  yanawapa washindi fursa ya kusoma nchini China. Picha hii ikionesha wanafunzi wanaosoma China wakitembelea karakana ya mafunzo ya utengenezaji bidhaa kwa kutumia teknolojia za akili bandia ya Chuo cha Kazi za Ufundi  wa Mashine na Umeme cha Zhejiang, China. (Picha na Yuan Junjie)

Kituo cha Elimu na Mafunzo ya Kazi za Ufundi cha Gabon Encock kilichojengwa na Kampuni ya China ya AVIC International. (Picha na He Deyu)

Kituo cha Elimu na Mafunzo ya Kazi za Ufundi cha Gabon Encock kilichojengwa na Kampuni ya China ya AVIC International. (Picha na He Deyu)

Kituo cha  Kitaifa cha Miradi ya Sayansi na  Teknolojia na Uboreshaji wa Uwezo wa Uvumbuzi  cha Uganda kilichojengwa na Kampuni ya China ya AVIC International. (Picha na Yu Pengfei)

Kituo cha Kitaifa cha Miradi ya Sayansi na Teknolojia na Uboreshaji wa Uwezo wa Uvumbuzi cha Uganda kilichojengwa na Kampuni ya China ya AVIC International. (Picha na Yu Pengfei)

Katika miaka ya hivi karibuni, kampuni za China zimeandaa mashindano ya ustadi wa kazi za ufundi katika nchi za Afrika na kuanzisha miradi ya elimu ya kazi za ufundi barani Afrika, hali inayosaidia nchi nyingi za Afrika kuboresha viwango vyao vya elimu ya kazi za ufundi, kuwezesha soko la elimu ya kazi za ufundi, na kusaidia nchi za Afrika kubadilisha idadi kubwa ya nguvukazi kuwa nguvu bora ya maendeleo ya nchi zao.

Makamu wa Rais wa Kenya Rigasi Gachagua alisema kuwa mashindano hayo yametoa mchango muhimu kwa ajili ya kusaidia vijana kuongeza ujuzi wao wa kazi za ufundi, na pia yataboresha tija na ushindani wa Kenya.

"Wanafunzi wamejifunza ujuzi mbalimbali katika mashindano hayo, ambao utawasaidia kufanya uvumbuzi na kuanzisha shughuli zao. Wakati huo huo, hii pia itasaidia Kenya kupunguza tatizo la uhaba wa nafasi za ajira na kupunguza umaskini."

Kuanzia Julai hadi Agosti 2023, Mashindano ya 8 ya Ustadi wa Kazi za Ufundi ya Afrika yaliyoandaliwa na Kampuni ya China Aviation Technology International Holdings (ambayo inajulikana kwa jina la "AVIC International"), kampuni tanzu ya Shirika la Usafiri wa Anga la China, lilifanyika Nairobi, Kenya, likivutia vikundi 83 na wanafunzi 332 kutoka nchi 9 zikiwemo Kenya, Cote d'Ivoire, na Misri.

"Kushiriki katika mashindano siyo tu kuwania tuzo, lakini pia kwa mustakabali mzuri wa Afrika." Ofisa wa Wizara ya Elimu na Michezo ya Uganda, Jane Egao-Oku alisema.

"Uganda inatumia elimu ya kazi za ufundi kama injini ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi na kuleta mageuzi. Mashindano ya Ustadi wa Kazi za Ufundi ya Afrika yanasaidia Uganda kuongeza uwezo wa wafanyakazi wake na kuandaa kundi la vijana wenye vipaji vya ujuzi ambao wanatarajiwa kuleta ufumbuzi mpya kwa changamoto zinazoikabili Afrika katika siku zijazo." ameongeza

"Kuwapa vijana wengi wa Afrika fursa ya kubadilisha maisha yao ya baadaye"

Huang Xuchen, Meneja Mkuu wa Mradi wa Idara ya Elimu ya Ufundi ya Kampuni ya AVIC International amesema, hadi sasa, washiriki karibu 1,300 kutoka vyuo na vyuo vikuu zaidi ya 300 katika nchi 10 zikiwemo Kenya, Misri, Uganda na Ghana wameshiriki kwenye mashindano hayo. Katika vyuo na vyuo vikuu hivyo, vyuo 9 vilipokea oda za uzalishaji zenye thamani ya Dola za Kimarekani 500,000 zilizotolewa na AVIC International, wanafunzi 24 wamepata fursa za kusoma nchini China, wanafunzi 45 wamepata mafunzo ya kazi za ufundi na nafasi za kazi katika Kampuni ya AVIC International, na washiriki 85 wamepata mafunzo ya kazi za ufundi kwenye kampuni za China katika nchi husika.

"Kiwango cha jumla cha ufundishaji wa shule kimeboreshwa sana"

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Elimu ya Kenya, hadi sasa, Mradi wa Kampuni ya Kimataifa ya AVIC wa Elimu ya Kazi za Ufundi nchini Kenya umetoa mafunzo kwa walimu zaidi ya 1,500 na wafanyakazi wenyeji wa kiufundi zaidi ya 60,000, na shule jumla ya 154 kutoka kaunti 47 nchini Kenya zimenufaika nao.

Mbali na Kenya, Kampuni ya Kimataifa ya AVIC pia inashirikiana na nchi za Afrika kama vile Uganda, Gabon, Ghana, Cote d'Ivoire, na Zambia kutafuta suluhu za elimu ya kazi za ufundi.

Hadi kufikia sasa, vyuo na vyuo vikuu 177 vimepandishwa hadhi na kukarabatiwa, vyuo vipya vitatu vya kazi za ufundi vimejengwa, na vyuo vingine 9 vya kazi za ufundi vinaendelea kujengwa.

Waziri Mkuu wa zamani wa Côte d'Ivoire, Patrick Assi, alisema kuwa baada ya kukamilika kwa mradi wa shule ya mafunzo ya kazi za ufundi wa Côte d'Ivoire uliojengwa na kampuni za China, utasaidia Côte d'Ivoire kuongeza vipaji zaidi vya kazi za ufundi, kuendana na mahitaji ya maendeleo ya baadaye ya viwanda, kupunguza matatizo ya ajira ya kundi la vijana, na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya nchi hiyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha