Rais Xi Jinping akutana na Rais wa Finland Sauli Niinisto kupitia njia ya video

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 11, 2024

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Finland Sauli Niinisto kupitia njia ya video mjini Beijing, China, Januari 10, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Finland Sauli Niinisto kupitia njia ya video mjini Beijing, China, Januari 10, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatano amekutana na Rais wa Finland Sauli Niinisto kupitia njia ya video akisema Finland ilikuwa moja ya nchi za kwanza za Magharibi kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China na kwa muda mrefu imekuwa ikifuata sera ya kirafiki kuhusu China.

"Rais Niinisto hasa amejikita katika kuhimiza ushirikiano wa kufuata hali halisi kati ya Finland na China na mawasiliano ya kirafiki katika nyanja mbalimbali, jambo ambalo nashukuru." Rais Xi amesema.

Amesema katika miaka ya hivi karibuni, uhusiano kati ya China na Finland umedumisha maendeleo thabiti, na ushirikiano wao katika sekta ya misitu, mazao ya kilimo na chakula, mawasiliano ya habari, nishati, ulinzi wa mazingira, sayansi na teknolojia, elimu, michezo ya majira ya baridi na nyanja nyinginezo umeendelezwa kwa kina siku hadi siku, ukileta manufaa halisi kwa watu wa nchi hizo mbili.

China ingependa kunufaika pamoja na Finland na fursa za maendeleo, kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana, kuendeleza kwa kina uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa aina mpya ulio wa kuelekea siku za baadaye, kuimarisha uratibu katika masuala ya kimataifa, kutetea kwa pamoja ushirikiano wa pande nyingi, kulinda biashara huria, na kutoa mchango wa hamasa kwa ajili ya kulinda amani na utulivu duniani na kuhimiza maendeleo ya kisasa ya nchi zote duniani, Rais Xi amesema.

Kwa upande wake Niinisto amesema bado ana kumbukumbu za wazi za ziara mbili za Rais Xi nchini Finland na ziara yake nchini China, na mazungumzo yote ya awali yameacha hisia kubwa kwake.

Ameongeza kuwa, uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa aina mpya ulio wa kuelekea siku za baadaye kati ya Finland na China, ambao waliutangaza kwa pamoja, umedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo na kupata matokeo ya kuhimiza juhudi katika ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Finland Sauli Niinisto kupitia njia ya video mjini Beijing, China, Januari 10, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Rais wa Finland Sauli Niinisto kupitia njia ya video mjini Beijing, China, Januari 10, 2024. (Xinhua/Liu Bin)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha