Rais wa Ecuador asema nchi yake iko katika “hali ya vita” na haitajisalimisha kwa magaidi

(CRI Online) Januari 11, 2024

Rais Daniel Noboa wa Ecuador amesema Ecuador iko katika “hali ya vita” dhidi ya makundi ya uhalifu ya kigaidi yanayohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya, pia ameapa kuwa Ecuador haitaridhia matakwa yao.

Noboa alipohojiwa na “Radio Canela” Jumatano huko Quito amesema, Ecuador iko katika mapigano ya kutumia silaha yasiyo ya kimataifa. Wanapigania amani ya nchi, pia wanapambana na makundi ya kigaidi yenye watu zaidi ya elfu 20 kwa sasa.

Serikali ya Ecuador Jumanne ilitoa amri ya kuwatambua wanachama wa makundi 22 ya uhalifu kuwa ni “magaidi”, na kutangaza kuwa nchi hiyo inaingia katika hali ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ya kutumia silaha, na kuruhusu vikosi vya silaha kupambana na makundi hayo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha