Timu za matibabu za China zapongezwa kwa kuendeleza huduma za afya Tanzania

(CRI Online) Januari 11, 2024

Serikali ya Tanzania imetoa shukrani kwa Serikali ya China siku ya Jumanne kwa kutuma timu za matibabu nchini humo kusaidia kuboresha huduma za afya kwa watu wa nchi hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu katika Wizara ya Afya ya Tanzania, Paschal Ruggajo amesema, katika miongo sita iliyopita, madaktari zaidi ya 1,500 wa timu za matibabu za China wametumwa nchini Tanzania, wameokoa maisha ya watu zaidi ya milioni 20 wa Tanzania waliopatwa na magonjwa mbalimbali, na pia wamesaidia kuziba mapengo mbalimbali ya kiteknolojia kwenye hospitali za nchini humo.

Bw. Ruggajo amesema hayo mjini Dar es Salaam alipokuwa akihutubia hafla ya kuaga timu ya 26 ya madaktari wa China na kukaribisha timu ya 27 kutoka China.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha