

Lugha Nyingine
Waziri wa Mambo ya Nje wa China kufanya ziara Misri, Tunisia, Togo, Cote d’Ivoire, Brazil na Jamaika
(CRI Online) Januari 12, 2024
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning amesema, Waziri wa Mambo ya Nje ya China Wang Yi atafanya ziara katika nchi za Misri, Tunisia, Togo, na Cote d’Ivoire kuanzia tarehe 13 hadi 18 mwezi huu.
Bi. Mao Ning amesema, huu ni mwaka wa 34 ambapo Afrika imekuwa ikiwa kituo cha kwanza cha ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China nje ya nchi kila mwaka mpya unapoanza.
Ameongeza kuwa, baada ya ziara hiyo barani Afrika, Wang Yi atafanya ziara katika nchi za Brazil na Jamaica kuanzia tarehe 18 hadi 22 mwezi huu.
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma