China yaitaka jumuiya ya kimataifa kuunga mkono Afrika Magharibi na eneo la Sahel

(CRI Online) Januari 12, 2024

Naibu mwakilishi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Balozi Dai Bing, ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kusaidia Afrika Magharibi na eneo la Sahel kufikia amani na utulivu, kupambana na ugaidi na kukuza uchumi.

Balozi Dai Bing amesema, tangu mwaka jana, nchi za kanda hiyo zimefanya jitihada kubwa kudumisha amani na utulivu, licha ya kuendelea kukabiliwa na matatizo na changamoto. Amesema hali ya kisiasa katika baadhi ya nchi hizo bado ni tete huku mivutano ya ndani ya kijamii ikiongezeka.

Balozi Dai ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa China inaziunga mkono nchi za kanda hiyo kutatua masuala yao ya ndani kupitia mazungumzo, ili kuweka msingi kwa amani na maafikiano. Ameongeza kuwa ni muhimu kuleta imani na matumaini kwa watu kupitia kuboresha utawala na kuimarisha mamlaka ya nchi.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha