China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana na Uswizi: Waziri Mkuu wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2024

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Uswizi Viola Amherd kwenye treni maalum kutoka Zurich hadi Bern, mji mkuu wa Uswizi, Januari 14, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Uswizi Viola Amherd kwenye treni maalum kutoka Zurich hadi Bern, mji mkuu wa Uswizi, Januari 14, 2024. (Xinhua/Rao Aimin)

BERN, Uswisi - China iko tayari kuimarisha ushirikiano wa kunufaishana katika nyanja mbalimbali na Uswisi ili kupata matokeo zaidi halisi, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema siku ya Jumapili wakati akifanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Uswizi Viola Amherd kwenye treni maalum kutoka Zurich hadi Bern, mji mkuu wa Uswizi.

Huku akieleza kuwa Uswisi ni miongoni mwa nchi za kwanza za Magharibi kuitambua Jamhuri ya Watu wa China, Waziri Mkuu Li amesema nchi hizo mbili zina historia ndefu ya ushirikiano wa kirafiki.

Uswizi siyo tu inajivunia mandhari nzuri ya mazingira ya asili lakini pia ina mazingira mazuri ya kiikolojia, uwezo unaoongoza wa uvumbuzi na bidhaa zenye ubora wa juu za "Made in Switzerland", amesema.

Waziri Mkuu Li amesema hivi sasa, China inasonga mbele na maendeleo ya kisasa ya China kwa njia ya pande zote na maendeleo yenye ubora wa juu, huku akiongeza kuwa China iko tayari kuimarisha mawasiliano na kufunzana na Uswizi.

Ameongeza kuwa kampuni za Uswizi zimeshiriki kwa pande zote katika mchakato wa mageuzi na ufunguaji mlango wa China katika miaka 40 na zaidi iliyopita, na kuchangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China na kujipatia manufaa yao makubwa.

“China itaendelea tu kufungua mlango wake zaidi kwa nje, ikikaribisha kampuni zaidi za Uswizi kuwekeza nchini,” ameongeza.

Kwa upande wake, Amherd amemkaribisha Li kwa ziara rasmi nchini Uswizi na kumjulisha hali ya kitaifa ya Uswizi na mila za majimbo mbalimbali wakati wakiwa safarini.

Amesema, Uswizi iko tayari kushirikiana na China ili kuimarisha mawasiliano kati ya watu wa nchi hizo mbili na kuongeza zaidi maelewano na urafiki kati ya watu wao.

Pande hizo mbili pia zimebadilishana maoni kuhusu uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, maendeleo ya kijani, utalii wa kitamaduni, michezo ya majira ya baridi, na mambo mengine, na kukubaliana kuongeza ushirikiano katika nyanja zinazohusiana.

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Uswizi Viola Amherd kwenye treni maalum kutoka Zurich hadi Bern, mji mkuu wa Uswizi, Januari 14, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

Waziri Mkuu wa China Li Qiang akifanya mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Uswizi Viola Amherd kwenye treni maalum kutoka Zurich hadi Bern, mji mkuu wa Uswizi, Januari 14, 2024. (Xinhua/Wang Ye)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha