Waziri wa Mambo ya Nje wa China atoa wito wa kufanyika kwa mkutano wa amani wa kimataifa ili kutatua suala la Palestina

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 15, 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry wakikutana kwa pamoja na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao mjini Cairo, Misri, Januari 14, 2024. (Xinhua/Wang Dongzhen)

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry wakikutana kwa pamoja na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yao mjini Cairo, Misri, Januari 14, 2024. (Xinhua/Wang Dongzhen)

CAIRO - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi siku ya Jumapili kwenye mkutano na waandishi wa habari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry katika mji mkuu wa Misri, Cairo ametoa wito wa kuitishwa kwa mkutano wa amani wa kimataifa wa pande zote, wenye mamlaka na ufanisi zaidi ili kuweka mwelekeo na dira ya utekelezaji wa suluhu ya Mataifa Mawili ili kutatua mgogoro kati ya Israeli na Palestina.

Wang, ambaye pia mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China ameeleza uungaji mkono wa China kwa ajili ya kurejeshwa kwa mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina haraka iwezekanavyo, mwishowe kufikia lengo la kuishi pamoja kwa amani kati ya Palestina na Israel, na kuishi kwa mapatano kati ya Waarabu na Wayahudi.

“China siku zote inashikilia haki na usawa wa kimataifa, ikishirikiana na nchi za Kiarabu na Kiislamu ili kukomesha migogoro na ghasia, imefanya kila iwezalo kulinda usalama wa raia, na kufanya juhudi za kuhimiza suluhu ya pande zote, ya haki na endelevu. kwa suala la Palestina mapema iwezekanavyo,” mwanadiplomasia huyo mkuu wa China amesema.

Wang pia ametoa pendekezo lenye mambo makuu manne la kusuluhisha mgogoro wa Ukanda wa Gaza. Kwanza, kipaumbele kikubwa kwa sasa ni kumaliza mgogoro huo wa Gaza haraka iwezekanavyo, pili, ni jukumu la kimaadili kuhakikisha utoaji wa haraka wa misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, tatu, matakwa ya watu wa Palestina lazima yaheshimiwe kikamilifu kuhusu mipango ya baadaye ya Gaza, na nne utekelezaji wa suluhu ya nchi mbili ndiyo njia pekee ya kufikia suluhu ya haki ya suala la Palestina.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha