Zambia yatangaza hatua zaidi za kukabiliana na kipindupindu

(CRI Online) Januari 15, 2024

Waziri wa Afya wa Zambia Bibi Sylvia Masebo amesema serikali ya nchi hiyo imetangaza hatua kali zaidi zinazolenga kudhibiti mlipuko wa kipindupindu.

Amesema serikali imewasilisha kifungu kwenye hati ya kisheria iliyotangazwa mapema ili kuimarisha hatua za kuzuia na kudhibiti ugonjwa huo.

Bibi Masebo amesema kifungu hicho cha sheria kilichoanzishwa pia kinapiga marufuku watu kutoka kwenye baadhi ya maeneo kuingia kwenye vituo vya matibabu ya kipindupindu, na kufanya mazishi salama kwa wanaoshukiwa kufa kwa ugonjwa wa kipindupindu.

Hatua nyingine za awali ni pamoja na marufuku ya biashara ya chakula kwenye mazingira machafu, marufuku ya mikusanyiko ya mazishi kwa watu wanaokufa kwa kipindupindu, na makanisa yanaruhusiwa kuendesha misa kwa muda wa saa mbili tu.

Hata hivyo licha ya hatua hizo idadi ya wagonjwa wapya bado ni kubwa, ambapo katika kipindi cha saa 24 zilizopita kulikuwa na wagonjwa wapya 431 na vifo 11.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha