Waziri wa Mambo ya Nje wa China asifu maendeleo makubwa katika uhusiano kati ya China na Tunisia miongo 6 iliyopita

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2024

Rais wa Tunisia Kais Saied (wa kwanza kulia mbele) na Wang Yi (wa kwanza kushoto, mbele), Waziri wa Mambo ya Nje wa China ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), wakitembelea maktaba ya Chuo cha Kimataifa cha Diplomasia cha Tunis huko Tunisia, Januari 15, 2024. Wang alihutubia hafla iliyofanyika katika mji mkuu wa Tunisia, Tunis siku ya Jumatatu kwa ajili ya kuzindua Chuo cha Kimataifa cha Diplomasia cha Tunis kilichojengwa na China, ambayo pia ilihudhuriwa na Rais Kais Saied wa Tunisia na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia, Nabil Ammar. (Xinhua/Huang Ling)

TUNIS - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amepongeza “urafiki mkubwa” uliofikiwa kati ya China na Tunisia katika miongo sita iliyopita tangu kuanzishwa kwa uhusiano wao wa kidiplomasia kwenye uzinduzi wa Chuo cha Kimataifa cha Kidiplomasia cha Tunis, kilichojengwa na China ambayo pia ilihudhuriwa na Rais wa Tunisia Kais Saied na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia, Nabil Ammar mjini Tunis, mji mkuu wa Tunisia.

Imechukua miaka minane kujenga chuo hiki, cha pekee cha aina yake ambacho kimejengwa kwa msaada wa China katika nchi ya Kiarabu, mwanadiplomasia huyo mkuu wa China ameeleza.

Wang, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) ameongeza kuwa, chuo hicho, ambacho kimeonyesha kiwango cha juu na ubora wa uhusiano kati ya China na Tunisia, kitakuwa ishara na jukwaa jipya la kuendeleza urafiki wa jadi kati ya China na Tunisia.

“Katika miongo kadhaa iliyopita, China na Tunisia zimeungana mkono kithabiti katika kulinda uhuru, mamlaka na ukamilifu wa ardhi, na kuchagua njia zao za maendeleo,” Wang amesema.

Katika hafla hiyo, Wang pia ametoa wito wa kujenga Dunia yenye usawa na utaratibu ya ncha nyingi na kuendeleza utandawazi wa kiuchumi unaojumuisha watu wote.

Kwa upande wake Ammar amesema mwaka huu inatimia miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tunisia na China ambao umepata mafanikio mazuri katika ushirikiano wa pande mbili katika nyanja mbalimbali.

Amesema, kuimarisha urafiki wa pande mbili ni matakwa ya pamoja ya kisiasa ya pande zote mbili na inaendana na maslahi ya pamoja ya nchi hizo mbili na watu wao.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha