

Lugha Nyingine
China kuendelea kuhimiza uhusiano wa pande mbili kati yake na Uswisi ili kupata matokeo halisi zaidi katika ushirikiano wa kunufaishana
Waziri Mkuu wa China Li Qiang akihudhuria hafla kubwa ya kumkaribisha iliyoandaliwa na Rais wa Shirikisho la Uswizi Viola Amherd huko Lohn Estate kabla ya mazungumzo yao mjini Bern, Uswizi, Januari 15, 2024. (Xinhua/Zhai Jianlan)
BERN, Uswizi - China iko tayari kuendelea kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa pande mbili kati yake na Uswisi ili kupata matokeo halisi zaidi katika ushirikiano wa kunufaishana, Waziri Mkuu wa China Li Qiang amesema siku ya Jumatatu kwenye mazungumzo na Rais wa Shirikisho la Uswizi Viola Amherd ambayo pia yalihudhuriwa na Chansela wa Serikali Kuu ya Uswisi Guy Parmelin, Mkuu wa Idara ya Serikali ya Masuala ya Uchumi, Elimu na Utafiti.
Tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia miaka 74 iliyopita, uhusiano wa pande hizo mbili umepata maendeleo makubwa na kuweka mambo mengi "ya kwanza," Li amesema.
Amekumbusha kuwa Mwaka 2016 Rais Xi Jinping wa China na kiongozi wa wakati huo wa Uswizi kwa pamoja walitangaza kuanzishwa kwa ushirikiano wa kimkakati wa kiubunifu kati ya China na Uswisi, ambao umetoa mwongozo muhimu kwa maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.
China iko tayari kushirikiana na Uswisi kutekeleza makubaliano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, kuimarisha zaidi msingi wa hali ya kuaminiana kisiasa na kuendeleza moyo wa ushirikiano wa "usawa, uvumbuzi na kunufaishana," Waziri Mkuu Li amesema.
Amesema China iko tayari kuendelea kusukuma mbele mawasiliano ya karibu ya ngazi ya juu kati yake na Uswizi, kutumia vyema utaratibu wa mazungumzo na ushirikiano kati ya serikali hizo mbili, na kuharakisha kurejesha mawasiliano katika ngazi mbalimbali na katika nyanja mbalimbali.
Amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano na Uswisi katika masuala ya mabaki ya utamaduni, elimu, vijana na michezo.
Kwa upande wao, Amherd na Parmelin wamesema Uswisi ni moja ya nchi za kwanza kuitambua Jamhuri ya Watu wa China, na kubainisha kuwa uhusiano kati ya Uswisi na China una historia ndefu na uhusiano mzuri, na ushirikiano wao wa kibiashara na uwekezaji umeendelea kuimarishwa licha ya athari za janga la UVIKO-19.
Wamesema Uswisi itaendelea kuhimiza mazungumzo yenye ubora wa juu ya pande mbili na China, kuzidisha ushirikiano katika nyanja kama vile uchumi, biashara, elimu, fedha, sayansi na teknolojia pamoja na mawasiliano kati ya watu na ya kitamaduni.
Waziri Mkuu wa China Li Qiang, akiambatana na Rais wa Shirikisho la Uswisi Viola Amherd, akikagua gwaride la heshima kwenye hafla ya kukaribishwa kwake huko Lohn Estate kabla ya mazungumzo yao mjini Bern, Uswizi, Januari 15, 2024. (Xinhua/Wang Ye)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma