Jamhuri ya Nauru yatangaza kuvunja "uhusiano wa kidiplomasia" na Taiwan

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 16, 2024

Picha hii iliyopigwa Januari 15, 2024 ikionyesha Bunge la Jamhuri ya Nauru. (Picha na Liang Bijiao/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Januari 15, 2024 ikionyesha Bunge la Jamhuri ya Nauru. (Picha na Liang Bijiao/Xinhua)

SYDNEY - Jamhuri ya Nauru imetangaza Jumatatu kwenye Mtandao wa Facebook, kwamba itatambua kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuvunja "uhusiano wa kidiplomasia" na Taiwan, ambapo imesema serikali ya Nauru itafuata azimio la Umoja wa Mataifa Namba 2758, linaloitambua Jamhuri ya Watu wa China kama serikali pekee halali inayowakilisha China nzima, na inaitambua Taiwan kama sehemu isiyoweza kutengwa ya ardhi ya China.

Nauru haitaendeleza tena uhusiano wowote wa kiserikali au mawasiliano ya kiserikali na Taiwan, imesema serikali ya nchi hiyo.

Na Rais wa Nauru David Adeang atatoa taarifa kuhusu suala hili katika kikao kijacho cha bunge, na kutoa hotuba kwa nchi nzima kwenye vituo vya televisheni na redio vya Nauru.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amesema China inafurahia na kukaribisha uamuzi wa serikali ya Jamhuri ya Nauru wa kutambua kanuni ya kuwepo kwa China moja, kuvunja kile kinachoitwa uhusiano wa kidiplomasia na Taiwan, na kuanzisha tena uhusiano wa kidiplomasia na China.

China ingependa kushirikiana na Nauru katika kufungua ukurasa mpya wa uhusiano wa pande mbili kwenye msingi wa kanuni ya kuwepo kwa China moja, amesema msemaji huyo.

Nauru ni nchi ya kisiwa katika Bahari ya Pasifiki ya Kati, yenye eneo lenye ukubwa wa ardhi ya kilomita za mraba 21.1 na wakazi wapatao 13,000.

Picha hii iliyopigwa Januari 15, 2024 ikionyesha Bunge la Jamhuri ya Nauru. (Picha na Liang Bijiao/Xinhua)

Picha hii iliyopigwa Januari 15, 2024 ikionyesha Bunge la Jamhuri ya Nauru. (Picha na Liang Bijiao/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha