

Lugha Nyingine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atoa wito wa kusimamisha vita huko Gaza katika siku 100 za vita
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya Gaza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Januari 15, 2024. (Loey Felipe/Picha ya Umoja wa Mataifa/ Xinhua)
UMOJA WA MATAIFA - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres Jumatatu tena ametoa wito wa kusimamisha vita mara moja huko Gaza wakati mgogoro huo unatimiza siku 100 akisema kuna suluhu moja tu ya kusaidia kushughulikia masuala yote ya kiwango kisicho na kifani cha vifo vya raia na hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza, hatma ya mateka, na mivutano ambayo inaenea katika eneo lote. "Tunahitaji usimamishaji wa vita mara moja wa kibinadamu."
Licha ya ukatili wa Gaza, hali ya mivutano katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu inazidi kupamba moto na kuongezeka kwa ghasia kunazidisha msukosuko mbaya wa kifedha ambao upo sasa kwa Palestina. Mivutano pia iko juu sana katika Bahari Nyekundu na kwingineko na hivi karibuni inaweza kuwa vigumu kuzuia, ameonya.
"Nina wasiwasi mkubwa kuhusu kushambuliana kila siku katika Mstari wa Bluu. Hii inahatarisha kuchochewa na kuenea zaidi kwa mgogoro kati ya Israel na Lebanon na kuathiri kwa kiasi kikubwa utulivu wa kikanda," amesema Guterres, huku akiongeza kuwa "Ni wajibu wangu kufikisha ujumbe huu rahisi na wa moja kwa moja kwa pande zote: Acheni kucheza na moto katika Mstari wa Bluu, punguzeni mivutano, na komesheni uhasama kwa mujibu wa Azimio la 1701 la Baraza la Usalama."
Ingawa kumekuwa na hatua kadhaa za kuongeza mtiririko wa msaada wa kibinadamu katika Gaza, misaada ya kuokoa maisha haipatikani kwa watu ambao wamevumilia miezi kadhaa ya kushambuliwa bila kukoma popote karibu na kiwango kinachohitajika. Kivuli kirefu cha njaa kinawaandama watu wa Gaza -- pamoja na magonjwa, utapiamlo na matishio mengine ya kiafya, amesema.
Pande husika lazima ziheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu, ziheshimu na kulinda raia, na kuhakikisha mahitaji yao muhimu yanakidhi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiongea na waandishi wa habari kuhusu hali ya Gaza kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Januari 15, 2024. (Loey Felipe/Picha ya Umoja wa Mataifa/ Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma