

Lugha Nyingine
Mkutano wa harakati ya Nchi zisizofungamana na Upande Wowote wafunguliwa nchini Uganda, Palestina na Israel kuwa ajenda kuu
Maofisa wakuu wa nchi wanachama wa harakati ya nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) wakiendelea na mkutano wa siku mbili ulioanza Jumatatu, wakitoa mwito suala la mgogoro wa Palestina na Israel kuwa ajenda muhimu.
Mkutano huo umefunguliwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda Azerbaijan ambaye pia ni mkuu wa ujumbe wa nchi hiyo kwenye mkutano huo Bw. Yalchin Rafiyev, ambaye amezitaka nchi wanachama kuendelea kuwa na umoja wakati dunia ikiendelea kukumbwa na changamoto zenye utatanishi.
Kwenye mkutano huo Balozi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Riyad Mnasour amewataka wajumbe wa mkutano huo kujadili mgogoro kati ya Palestina na Israel, na kusema kuwa licha ya kuwa Harakati hiyo inakumbana na changamoto nyingi, mgogoro huo wa mashariki ya kati ni wa haraka zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma