Chama tawala cha Tanzania chateua katibu mkuu mpya

(CRI Online) Januari 16, 2024

Chama tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi (CCM), kimemteua mwanadiplomasia Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Daniel Chongolo Novemba 2023.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Bw. Paul Makonda amemtangaza Bwana Nchimbi ambaye ni mwanadiplomasia na aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uwaziri wa Serikali ya Tanzania ikiwemo nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani kuwa ameteuliwa kuwa katibu mkuu mpya.

Bw. Makonda pia ameuambia mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wa siku moja wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliofanyika Zanzibar kuwa Bw. Nchimbi amepitishwa na wajumbe wa mkutano huo baada ya jina hilo kupendekezwa na Kamati Kuu ya chama hicho.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha