

Lugha Nyingine
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa China na Tunisia wasisitiza maendeleo ya kujitegemea
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia Nabil Ammar mjini Tunis, Tunisia, Januari 15, 2024. (Xinhua/Huang Ling)
TUNIS - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi na mwenzake wa Tunisia Nabil Ammar, wameeleza nia yao ya kuungana mkono kwa ajili ya maendeleo ya kujitegemea ya kila upande kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika Tunis, mji mkuu wa Tunisia siku ya Jumatatu.
Wang, ambaye pia Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema mwaka huu ni maadhimisho ya kutimia miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tunisia, na hivyo kuwa na umuhimu mkubwa katika kuunganisha siku zilizopita na zijazo.
"Tuko tayari kuchukua fursa hii kufanya kazi na Tunisia kudurusu uzoefu wa mafanikio na kukuza urafiki wetu wa jadi ili kuandika ukurasa mpya wa ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Tunisia," amesema.
Pande hizo mbili zinahitaji kusaidiana katika masuala yanayohusu maslahi ya kimsingi na mambo makuu yanayofuatiliwa ya kila upande, ili kutoa msingi thabiti na nguvu kubwa kubwa katika uhusiano wa pande mbili, ameongeza.
Wang amesema Fikra ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye Umaalum wa China kwa Zama Mpya, inatoa mwongozo wa kimsingi wa kuijenga China kuwa nchi kubwa na kwa lengo kubwa la Ustawishaji wa Taifa la China kupitia maendeleo ya kisasa ya China.
Wang amesema China itahimiza maendeleo ya kisasa ya Dunia kwa kutumia maendeleo ya kisasa ya China, na iko tayari kubadilishana uzoefu katika uongozi na Tunisia na kuongeza uwezo wa Tunisia wa maendeleo ya kujitegemea ili kupata maendeleo na ustawi wa pamoja.
Kwa upande wake, Ammar amesema kuwa Tunisia na China, zikichangia maslahi na maadili ya pamoja, zina msingi imara wa kisiasa, kasi nzuri ya maendeleo, na ushirikiano wenye hamasa unaleta uhusiano wa pande mbili.
Tunisia inathamini urafiki wake na China na daima utakumbuka uungwaji mkono na msaada wa China.
Ammar amesisitiza kuwa Tunisia daima inashikilia kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China Moja na iko tayari kufanya kazi na China kusukuma mbele maendeleo zaidi ya uhusiano wa pande mbili.
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni Mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), akifanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia Nabil Ammar mjini Tunis, Tunisia, Januari 15, 2024. (Xinhua/Huang Ling)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma