Umoja wa Mataifa kuchapisha stempu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2024

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2024

Picha hii iliyotolewa na Shirika  la Posta la Umoja wa Mataifa (UNPA) Januari 16, 2024 ikionesha stempu za mwaka wa Dragoni. UNPA itatoa  stempu hizo za shughuli maalum ili kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China kwa kalenda ya kilimo ya China. (Picha kwa hisani ya UNPA/Kutumwa Xinhua)

Shirika la Posta la Umoja wa Mataifa (UNPA) litatoa stempu za shughuli maalum kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China utakaowadia.

Taarifa kutoka shirika la UNPA imesema, stempu hizo zitatolewa siku ya Ijumaa wiki hii, kila seti ina stempu 10 zenye thamani ya Dola za Marekani 1.5 kila moja, na kila stempu ni yenye picha ya dragoni anayeruka mawinguni, kwa kuwa mwaka 2024 kwa kalenda ya kilimo ya China utakuwa mwaka wa dragoni.

Mnamo mwaka wa 2021, Shirika la UNPA lilikamilisha kazi yake ya uchapishaji wa stempu zenye wanyama 12 ambao kila mnyama anawakilisha mwaka mmoja kwa mzunguko wa miaka 12. Stempu mpya ya dragoni ni stempu ya tatu katika uchapishaji wa stempu wa shirika hilo kwa ajili ya kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China.

Mwaka mpya wa jadi wa China, ambao huitwa Sikukuu ya Spring, ni sikukuu muhimu zaidi kwa Wachina wanaoishi katika sehemu mbalimbali duniani. Sikukuu hiyo ya mwaka huu itakuwa tarehe 10, Februari.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha