

Lugha Nyingine
Ufundi wa kupanda mpunga wa China wanufaisha watu wa Cote d'Ivoire
Wakulima wa mpunga wakivuna mpunga katika eneo la upandaji wa mpunga wa Gegedou la Mkoa wa Divo, Cote d'Ivoire, Januari 8. (Picha na Han Xu/Xinhua)
Mwaka 1997, eneo la kilimo la Gegedou lilikaribisha Timu ya kwanza ya Ushirikisho wa Ufundi wa Kilimo ya China. Ukiwa ni mradi wa kwanza wa seti ya kilimo baada ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Cote d'Ivoire, baada ya juhudi zilizofanywa kwa karibu miaka 30 na timu 11 za wataalam wa kilimo, hivi sasa eneo la kilimo la Gegedou sio tu ni kituo cha vielelezo vya kilimo cha China na Cote d'Ivoire, bali pia limekuwa kituo cha upandaji wa mpunga kinachojulikana nchini Cote d'Ivoire.
Mkulima wa mpunga akiendesha mashine kuvuna mpunga katika eneo la kilimo la Gegedou la Mkoa wa Divo, Cote d'Ivoire, Januari 8. (Picha na Han Xu/Xinhua)
Mtaalam Zhang Jing wa Timu ya Ushirikisho wa Ufundi wa Kilimo ya China nchini Cote d'Ivoire, alisema kuwa timu hiyo imethibitisha aina 4 za mpunga nchini Cote d'Ivoire, ambazo zote zimeinua kwa kiasi kikubwa utoaji wa mazao, sifa bora na ladha nzuri zikilinganishwa na aina za jadi za sehemu za huko, miongoni mwao, uzalishaji wa mpunga wa aina ya C26 umefikia tani 7 kwa kila hekta na imeenezwa nchini kote Cote d'Ivoire.
"Kila mwaka inapofika wakati muhimu wa uzalishaji, tutawakusanya wakulima wa eneo la kilimo kwenye mashamba ya majaribio kutoa mafunzo ana kwa ana na kuwafundisha hatua kwa hatua. Wakulima wengi kutoka mikoa mingine pia wanaweza kuja kujifunza." Zhang Jing aliwaambia waandishi wa habari.
Wataalam wa Timu ya Ushirikisho wa Ufundi wa Kilimo ya China wakitoa mafunzo kwa wakulima wa mpunga katika eneo la kilimo la Gegedou la Mkoa wa Divo, Cote d'Ivoire, Tarehe 29, Aprili, Mwaka 2023. (Picha iliyotolewa na Timu ya Ushirikisho wa Ufundi wa Kilimo ya China nchini Cote d'Ivoire)
Kwa kupitia mafunzo ya miaka mingi, wakulima wengi wa Afika wametumia ufundi waliojifunza kutoka kwa China wakipanda mpunga wameongeza uzalishaji wa mpunga na mapato ya familia, pia wamewahimiza wakulima wa vijiji jirani kupanda mpunga pamoja. Kuibuka kwa makundi ya wakulima wa mpunga, wasimamizi wa mpunga, na waendeshaji mashine za kilimo kumeongeza sana nafasi za kazi na kuimarisha kilimo cha mpunga nchini Cote d'Ivoire.
Mwenyekiti wa Shirika la Kilimo la Mpunga la Eneo la Kilimo la Gegedou alisema kuwa wataalam wa kilimo wa China wameleta aina bora za mpunga zenye uzalishaji mkubwa na ufundi wa kisasa wa upandaji wa kilimo, na kuwawezesha wakulima wa Cote d'Ivoire kupata chakula salama na kuwanufaisha sana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma