Wanasayansi wa Kenya wazindua dawa ya kupunguza malaria miongoni mwa wanawake wajawazito walio na VVU

(CRI Online) Januari 17, 2024

Dawa mpya inayotarajiwa kupunguza maambukizi ya malaria miongoni mwa wanawake wajawazito wanaoishi na VVU, imetolewa Jumanne na wanasayansi wa Kenya na Malawi kufuatia majaribio makini.

Kupitia matokeo ya utafiti yaliyochapishwa katika jarida la linaloheshimiwa la Lancet, wanasayansi hao wamebainisha kuwa kuongezwa kwa dawa ya kutibu malaria (dihydroartemisinin-piperaquine) kwenye orodha ya dawa nyingine zilizopo, kutapunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuambukizwa malaria miongoni mwa wanawake wajawazito wanaoishi na VVU.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Tiba ya Kenya (KEMRI), Bw. Elijah Songok amesema hayo ni mafanikio makubwa yanayoongeza dawa dhidi ya ugonjwa unaohatarisha asilimia takriban 70 ya maisha ya wagonjwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha