Tanzania na Angola zasaini hati za makubaliano kuongeza ushirikiano

(CRI Online) Januari 17, 2024

Serikali za Tanzania na Angola zimesaini hati tatu za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta ya mafuta na gesi, kuondoa visa kwa raia wa nchi hizo wenye hati za kusafiria za kidiplomasia na za kikazi pamoja na ushirikiano katika sekta ya afya.

Makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Makamba, Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Angola, Balozi Téte António kwenye Mkutano wa Pili wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Angola uliomalizika jana Jumanne Visiwani Zanzibar.

Viongozi hao pia wamekubaliana kuyafanyia kazi masuala mbalimbali hususan kuanzisha safari za ndege za moja kwa moja kutoka Dar es Salaam hadi Luanda, kuandaa kongamano la bishara na uwekezaji, na kuziwezesha sekta binafsi kufanya kazi kwa pamoja.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha