Rais Xi Jinping ampongeza Felix Tshisekedi kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa DRC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 18, 2024

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping Jumatano amempongeza Felix Tshisekedi kwa kuchaguliwa tena kuwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) akieleza kuwa DRC na China zinafurahia urafiki wa kijadi na ni washirika wenzi wa kimkakati wa pande zote na kwamba uhusiano wa pande mbili katika miaka ya hivi karibuni umeendelea kwa kasi ukiwa na ushirikiano wa kivitendo wenye manufaa na kuzidisha urafiki wa kijadi.

Rais Xi amesema angependa kushirikiana na Rais Tshisekedi katika kuongeza hali ya kuaminiana kisiasa kwa pande zote, kustawisha uhusiano wa nchi hizo mbili ulio wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote, na kusukuma mbele maendeleo mapya na makubwa zaidi ya ushirikiano kati ya China na DRC. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha